#PART#THREE :-
3: Kanuni ya kutilia mkazo au kujipa sharti (commitment) na kuweka mwelekeo eneo moja pasipo kuhamia eneo lingine. (focus)
Mwalimu wa masuala ya kiroho na mafanikio Shemeji Melayeki aliwahi kuelezea habari moja iliyokuwa ikijieleza kama ifuatavyo, mtu mmoja aliwahi kujisifia jinsi alivyo na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja, jamaa mmoja aliyekuwa pembeni yake akimsikiliza akacheka sana. Akamuuliza, “Kwani vipi mbona umecheka?” Akamjibu “Unafanya chochote ndiyo maana hauwi lolote, huu ni mwaka wa 15 hatukufahamu kwa lolote wala hatujui tukutambue kama nani?” Ndivyo ilivyo kwa watu wengi wanajaribu kufanya kila kitu pasipo kuweka mkazo na mwelekeo kwenye eneo moja ili watambulike katika hilo na badae kuweza kuwapa matokeo makubwa.
Melayeki anaendelea kusema, huwezi kuwa nyota wa michezo yote duniani, lazima utafute eneo moja ambalo utakuwa kinara, bingwa, mtaalamu, nguli, mkuu, kiongozi kwenye eneo hilo. (You can’t be the superstar of all sports and games around the world, find your niche and be the best ever). Huwezi kupanda juu kwa kung’ang’ania ngazi kumi, kadri mambo unayofanya yanavyozidi kuwa mengi ndivyo ufanisi wako unavyopungua. Amua kushikilia kile unachokifanya leo hadi uone matokeo kisha uamue kwa dhati kuamia jambo lingine.
Leo amua kuanza kufanya jambo ulilotaka kulifanikisha kwa muda mrefu, kwa kutumia kanuni nilizokufundisha hapo juu ukiamini hakuna linaloshindikana. Amini ndoto yako inawezekana.
Finishing out All Star weekend, Team LeBron defeats Team Giannis and Kevin Durant takes home MVP, while Hamidou Diallo wins dunk contest, and Joe Harris wins 3PT #nba#allstar#competition#stars#dunk#three